MJUE SAMAKI NYANGUMI (WHALE)


Duniani kuna mambo ambayo kamwe hungedhani kama yapo katika dunia hii,leo nimeamua kukuletea makala kuhusu samaki yangumi.


Tiririka.


Inasadikika kuna aina zaidi ya kumi na tisa za nyangumi ambao wametofautiana kwa sifa ikiwemo ukubwa na uzito na mambo mengine kadha wa kadha ikiwemo majina, lakini leo tuanze na nyangumi maarufu kabisa ambaye anafahamika kama “THE BLUE WHALE”. (NYANGUMI WA BLUU)


Yafuatayo ni mambo kadhaa usiyoyajua kuhusu nyangumi;


Nyangumi wa bluu (the blue whale) ndiye mnyama mkubwa kuwahi kutokea duniani.


Ulimi wa nyangumi ni sawa au zaidi ya tembo mkubwa.


Moyo wa nyangumi ni sawa au zaidi ya gari kwa uzito.


Nyangumi mkubwa anakula kilo elf thelathini na sita 36,000kg za samaki aina ya krill kila siku.


Nyangumi ana uwezo wa kuogelea kwa kasi ya kilomita nane kwa saa 8km/h na anaweza kuongeza kasi hadi kufikia kilomita thelathini na sita kwa saa 36km/h. Kwa madereva wa vyombo vya moto mnajua mwendo wa spidi thelathini na sita kwa saa upoje.


Nyangumi anaweza kuruka kwa umbali wa mita mia tano kwenda juu 500m. yaani jaribu kuzipiga hatua za kawaida 500 alafu fanya kama unazipiga kwenda juu.


Licha ya ukubwa wa nyangumi, anaweza kujeruhiwa na papa hadi kufa pia adui mwingine wa nyangumi ni meli kubwa ambazo zimekua zikiwajeruhi hadi kupoteza maisha kila mwaka.


Nyangumi ana uwezo wa kutunza lita elf tano za maji 5000litres mdomoni mwake kabla ya kuyatema nje.


Licha ya kua nyangumi anafanya mawindo yake kwenye kina kirefu lakini ni lazima arudi juu kupumua kabla ya kurudi tena chini ya maji.(Kumbuka nyangumi ana uwezo wa kutunza pumzi kwa dakika tisa 9 chini ya maji)


Nyangumi jike anaenda mwezini mara moja tu kwa miaka mitatu. Kumbuka nyangumi ni mamalia na anazaa.


Yai la nyangumi jike linatengenezwa kwa muda wa miezi kumi na moja au mwaka mmoja. Sio kama dada zetu kila mwezi yai linatengenezwa.


Kwa kawaida nyangumi jike ana uwezo wa kuzaa mara moja pekee na ndio maana idadi ya nyangumi ni ndogo sana duniani ukilinganisha na samaki wengine.


Mtoto wa nyangumi bluu anazaliwa akiwa na uzito wa kilo elf ishirini na saba 27000kg na urefu wa mita nane 8m.


Nyangumi watoto wanasaidiwa na mama zao kupumua kwa kurushwa juu ya maji na mama zao hii inawasaidia kuvuta hewa kabla ya kurudi chini ya maji.


Mtoto wa nyangumi ananyonya lita mia sita 600litres kwa siku, na anaongeza kilo tisini 90kg kila siku kwa mwaka wake wa kwanza. Hebu piga hesabu kilo tisini mara mia tatu sitini na tano utapata jibu nyangumi mwenye mwaka mmoja anakua na kilo ngapi? 365x90=?


Nyangumi wa bluu wanaogelea katika makundi madogo madogo na mara nyingi kila nyangumi huogelea kivyake.


Huwezi kumsikia nyangumi lakini huyu ndiye mnyama mwenye sauti kuliko wote duniani.


Nyangumi wana uwezo wa kuelewana hadi katika umbali wa kilomita elf moja na mia sita 1600km.


Pia nyangumi ana hisia kama binadamu na anaweza kuomba masamaha na kusema asante.


Inakadiriwa nyangumi elf kumi hadi elf ishirini na tano wanaogelea sasa katika bahari tofauti duniani. Idadi hii ni ndogo sana ulilinganisha na bahari zilizopo duniani na ukubwa wake.


Nyangumi bluu anaweza kuishi kwa wastani wa miaka 80-90, lakini miaka hio inaweza fika hadi 110.


Nyangumi anaweza fika uzito wa 180,000kg. watu wa mahesabu mtatupigia hapa nyangumi ana uzito wa tani ngapi ikiwa 1ton=1000kg.


Jina la kisayansi la nyangumi bluu ni balaenoptera musculus.


Aina nyingine za nyangumi ni fin whale,sei whale,humpback whale,bowhead whale,north atlantic right whale. Na kadha wa kadha.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post