SIMBA KUSHUSHA STRAIKA WA MAGOLI JANUARY.



“Nahitaji mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga kwani timu yangu inatengeneza nafasi nyingi za kufunga zinapotea, nikimpata huyo na straika mapema kabla ya dirisha dogo la usajili naimani tutakuwa na mabadiliko ndani ya timu yetu,”


“Tayari kuna mastraika tumewaona na tumeanza kuwafanyia kazi ya kuwaangalia na kuwafuatilia naimani kuna mmoja atatuvutia zaidi na tutakubaliana kumleta hapa kwetu,”


“Ukiangalia mechi zetu anatumika, Phiri Moses anafanya vizuri kwenye nafasi hiyo lakini kiasili eneo ambalo amekuwa akicheza ni nyuma ya mshambuliaji, lazima tulete straika dirisha dogo la usajili,"


“Kulingana na mazingira yalivyo wakati huu bado kuna nafasi ya kumtumia nahodha, John Bocco na Habibu Kyombo naimani wananafasi ya kutupa kitu bora kwenye kufunga kwani hawa wote ni wachezaji wa Simba,”


JUMA MGUNDA,Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC 🇹🇿.



Post a Comment

Previous Post Next Post