UJUE UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE

 

*


Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.


Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.


AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO


Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

1.Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa


2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) 

– Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)


CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO


Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;


Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)


Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)


Kuwa na mawazo mengi


Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi


Kunywa pombe na vinywaji vikali


Uvutaji wa sigara


Kuto kula mlo kwa mpangilio


DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO


Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama;


 Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula


Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo


Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa


Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu


Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu


Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito


Kushindwa kupumua vizuri


JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO


Kunywa maji mengi


Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo


Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)


Usivute sigara


Punguza au acha kunywa pombe


Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali


Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9


TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO


Tatizo la Vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post