AFISA POLISI MSTAAFU WA MAREKANI AZAMA KWENYE PENZI LA MMASAI HUYU

Mapya yaibuka ! Pichani mwanamama Deborah(60) ambaye ni afisa mstaafu wa jeshi la polisi nchini Marekani ameolewa na kijana huyo wa Kimasai toka Tanzania kwa jina la Saitoty Babu(30)


Akielezea, Deborah amesema mwaka 2017 aliingia Zanzibar yeye na binti yake kwa jina la Royce(30) ndipo wakiwa ufukweni wakaona vijana wawili wa kimasai mmojawapo akiwa ni huyo Saitoty. Kwasababu katika maisha yake hakuwahi kukutana na mtu toka jamii ya kimasai hasa aliyevaa kimasai, Debora aliomba kupiga nao picha kama ukumbusho, Saitoty akaomba atumiwe hiyo picha na ndipo akayapata mawasilianao ya Deborah wakawa wanawasiliana


Deborah alirudi kwao Califonia, Marekani lakini Saitoty akawa anawasiliana nae na kugusia kutaka kumuoa Deborah ambaye hakumpatiliza Saitoty hasa kwasababu wamepishana sana umri kwa miaka 30 na yeye binafsi Deborah japo alikuwa single lakini alikuwa anaishi kwa furaha. Haikuchukua miezi hata mitano Deborah alikuja kutalii tena Tanzania wakaonana tena. 


Siku moja Deborah akiwa anawasiliana na Saitoty kwa FaceTime, akamuonesha kwa watoto wake wengine wawili, wa kike Tiffany(32) na wa kiume Sherrick(27) ambao hawakuwa na hiana mama yao kuolewa na Saitoty sana sana walimuambia umri sio kigezo kama kakupenda na unaona mkiwa pamoja utakuwa na furaha basi sio mbaya kuolewa nae


Ambapo walifunga ndoa ya kimasai nchini Tanzania mwaka 2018 na mwaka huu 2022 ndio wamefunga ndoa ya kiserikali ila Deborah bado ana matumaini watafanya sherehe kubwa kwa mujibu wa mila za kimasai ili familia zote mbili zijumuike. Pia amepewa jina la Kimasai anaitwa Nashipai na ameanza kutumia jina la mume wake huyo yaani Deborah Nashipai Babu


Baada ya kufunga ndoa, Debora amehamia Tanzania na wanaishi katika nyumba ya udongo(boma) na mume wake huyo maeneo ya Ubena. Deborah amesema maisha ya Marekani na Tanzania yanatofautiana sana ila bado anafurahia kuishi Tanzania licha ya kwamba kwasasa anapikia kwa kutumia kuni na maji walipo ni shida kidogo. Pia eneo wanaloishi kwasasa wanajenga Lodge


Changamoto ya penzi lao amesema ni watu baki au wananzengo kuwakalia kooni kwa kusema Saitoty amemuoa Deborah ili apate uhalali wa kwenda kuishi Marekani(green card)
 

Post a Comment

Previous Post Next Post