AMCHOMA MWANAE KISA KAIBA DAGAA


 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Somoe Mohamed (34) Mkazi wa Dihimba Wilaya ya Mtwara kwa kosa la kumchoma moto katika viganja wa mikono yote Mtoto wake wa miaka mitano ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Namanjele.


Tukio hilo lilitokea tarehe 30/09/2022 majira ya saa 16:00 huko kijiji cha Namanjele ambapo Mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa kuweka nyasi kavu katikati ya viganja vya mikono ya Mtoto huyo kisha akamfunga kamba mikononi na kuwasha moto kwa kutumia kiberiti.


Mtoto huyo alifanyiwa ukatili huo baada ya kutuhumiwa kuiba/kudokoa dagaa na kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mtwara Vijijini na anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula.

Post a Comment

Previous Post Next Post