AHUKUMIWA JERA MIAKA 13 KWA KOSA HILI

😳😢 Kris Wu(32) ahukumiwa jela miaka 13 kwa makosa ya ubakaji na ukwepaji kulipa Kodi


Mwanamuziki huyo wa Canada mzaliwa wa China, amehukumiwa nchini China ambako alikuwa akifanya kazi zake za muziki baada ya kupatikana na makosa ya kuwabaka wanawake watatu waliokuwa wamelewa alienda nao nyumbani kwake. Pia amepatikana na hatia ya kuhadaa wanafunzi wa kike kufanya nao ngono huku wengine wakiwa chini ya miaka 18 na mmoja wa wanafunzi 2021 alijitokeza hadharani kumlalamikia Wu


Pia amepatikana na hatia ya kuficha kipato chako toka kwa watu na makampuni aliyokuwa akifanya nayo azi na hibyo pia kukwepa kulipa Kodi halali ya serikali n hini China ikiwemo kulipa Kodi chini ya kiwango kinachotakiwa


Licha ya kuhukumiwa miaka 13 jela mwanamuziki huyo ambaye pia ni mwigizaji na mwanamitindo ametakiwa pia kulipa dola za kimarekani milioni $83.77 ambazo ni zaidi ya bilioni 193 za Tanzania 


Wakati alipokamatwa na vyombo vya dola star huyo alikuwa ni balozi wa brands za makampuni 15 makubwa yakiwemo Bulgari, Lancome, Louis Vuitton and Porsche ambapo makampuni karibia yote yalitengua mikataba ya kufanya nae kazi baada ya kutiwa kizuizini na sasa amehukumiwa baada ya kupatikana na hatia
 

Post a Comment

Previous Post Next Post