DIAMOND PLATINUM AKIRI KUSUMBULIWA NA UGONJWA HUU


 Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye staa wa muziki wa kimataifa wa Tanzania, Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amezungumzia afya na mwonekano wa mwili wake na kusema kuwa hata yeye haelewi ni kwa nini kila siku anazidi kupungua.


Katika moja ya picha ambazo msanii wake, Mbosso Khan ameposti, Diamond amefika na kuonesha kushangaa kwake kutokana na kuendelea kupunguka kwa mwili wake na kila siku kuonekana kama kitoto.


Diamond anasema kuwa si yeye tu anazidi kushangaa kutokana na mabadiliko hayo ya mwili wake bali pia hata Watanzania wote wamekuwa wakiibua maswali kama hayo.


“Halafu nimekuwa mdogo, kila siku nazidi kuwa mdogomdogo. Hilo suala linawachanganya Watanzania wengi,” anasema Diamond.

Hata hivyo, jibu la Mbosso ndilo limewaacha wengi katika gumzo kubwa kwani walionekana kutolielewa.


Kwa kawaida wengi wanamjua Diamond kuwa wa miaka chini ya arobaini, lakini kwa jibu la Mbosso alionekana kudokeza kuwa msanii huyo tajiri wa Lebo ya WCB ana miaka zaidi ya 40 hivi.


“Kweli kaka kama huna miaka 40 vile safi sana,” Mbosso aijibu na kuwaacha wengi kwenye mataa.


Kama unatilia shaka kuhusu kupungua kwa uzito wa mwili wa Diamond Platnumz, ingia kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii na upate kutathmini.


Mjadala wa Diamond kupukutika ulianza muda mrefu tangu aliyekuwa msanii wake, Harmonize alipodai bosi wake huyo wa zamani kuna vitu vinamfanya kupukutika mwili.

Post a Comment

Previous Post Next Post