PANYA WATUHUMIWA KULA BANGI KILO 200 ILIYOKAMATWA







Polisi nchini India wameieleza mahakama nchini humo kuwa bangi zaidi ya kilo 200 waliyoikamata kama ushahidi kutoka kwa wahalifu imeliwa na Panya

Katika taarifa ya Polisi iliyosomwa ndani ya mahakama ya nchi hiyo inaeleza kuwa kesi tatu za matumizi ya bangi zimeshindwa kuendelea kutokana na Panya kula bangi hiyo ambayo ilihifadhiwa kama ushahidi

Jaji wa mahakama ya nchi hiyo Sanjay Chaudhary amesema baadhi ya kesi zimekwama kutokana na polisi kuwalaumu Panya kwa kula bangi waliyohifadhi vituoni

Polisi wanasema hawana utaalamu wa kushughulikia suala hilo kwani panya hao ni wadogo mno huku wakisema njia pekee ya kulinda bangi iliyokamatwa isiliwe na Panya ni kuipiga mnada kwa maabara za utafiti na makampuni ya dawa ili serikali ipate mapato.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya madawa nchini humo wamepinga madai hayo wakisema kwamba wanyama hao hawana uwezo wa kufanya jambo hilo na kama ingetokea basi panya wengi wangekutwa wamefariki katika maeneo hayo

 
 

Post a Comment

Previous Post Next Post