HATA NIKIFA LEO NITABAKI NAMBA MOJA - HARMONIZE

 


Staa wa Bongo Fleva wa kuitwa Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amejivunia mafanikio ya albam yake mpya ya Made For Us.


Albam hiyo ya tatu ya bosi huyo wa Lebo ya Konde Music Worldwide yenye nyimbo 14 imefanikiwa kupata streams zaidi ya milioni tatu kwenye mtandao wa Boom Play katika kipindi cha wiki mbili pekee.


Harmonize au Konde Boy amesherehekea mafanikio hayo makubwa na kubainisha kuwa yamemfanya apate hisia za ushindi.

|Hata nikifa leo, najua ninavyohisi kuwa nambari moja kwenye mchezo,” anasema Harmonize.

Mwamba huyo amejipiga kifua kuwa hakuhitaji promosheni ya vyombo vya habari, matangazo mengine yoyote wala machawa kufanikisha ushindi huo.


|Ni Mungu pekee na watu wazuri waliofanikisha,” anasema Konde Boy au Jeshi.


Staa huyo mkubwa nchini Tanzania pia anatamba albam yake hiyo kuongoza nchini Tanzania kwenye mtandao wa Audio Mack.

Harmonize aliachia albam ya Made For Us mwishoni mwa mwezi Oktoba, ikiwa ni albam yake ya tatu hadi sasa.


Ngoma zinazopatikana ndani ya albam hiyo ni pamoja na Mwenyewe, My Way, Leave Me Alone, Wote, Nitaubeba, Utanikumbuka, I Miss You, Die, The Way You Are, Miss Bantu, Best Friend, Deka, Too Much na Amelowa.


Harmonize anatoa shukran zake za dhati kwa mchumba wake, Kajala Masanja kwa kumsaidia katika utayarishaji wa albam hiyo.

“Umeifanya akili yangu iwe na utulivu, naweza kutunga mistari inayostahili. 


Ulifanya kazi kubwa zaidi kuboresha albam hii. Asante na nakupenda, mke wangu na bosi wangu,” Harmonize alimwambia Kajala.


Konde Boy anawasanua kwamba albam hiyo huenda ikawa ndiyo yake ya mwisho kuifanya kwa lugha ya Kiswahili.

Post a Comment

Previous Post Next Post