BUNGE LAMPA MAJALIWA MILIONI 5

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamechanga zaidi ya shilingi milioni tano kwa ajili ya kumpa kijana Majaliwa Jackson kama pongeza kwa ushujaa aliouonesha wakati wa ajali ya ndege ya Precision Air.


Fedha hizo zimechangwa baada ya Mbunge wa Nzega Vijijini Hamisi Kigwangalla kuomba mwongozo wa Spika endapo wabunge wanaweza kuchanga fedha hizo.

Majaliwa amefika bungeni jijini Dodoma kufuatia mwaliko wa Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato.

Katika ajali hiyo ya ndege iliyotokea tarehe 6 mwezi huu mkoani Kagera, Majaliwa alisaidia kuokoa watu 24 kutoka ndani ya ndege hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post