RONALDO NA MESSI WATOKEA KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKICHEZA MCHEZO HUU

Inaweza kuwa picha bora ya karne ???? Mastaa wawili wa soka ambao wamekua wakishindanishwa kwa miaka mingi Lionel Messi na Cristiano Ronaldo leo wametokea kwenye picha ya pamoja ya nje ya uwanja wakicheza mchezo wa chess zikiwa zimebaki saa chache kabla ya Kombe la Dunia kuanza.


Wapinzani hao wa muda mrefu walishiriki katika upigaji picha ya tangazo la Brand maarufu ya Louis Vuitton ambayo hujihusisha kutengeneza bidhaa mbalimbali za kifahari na za gharama kama mabegi, viatu na saa.


Kwenye picha hii ya tangazo la Louis Vuitton Wakali hawa wameonekana wakicheza mchezo wa chess juu ya mabegi mawili ya Louis na wote wameipost picha hiyo kwenye mitandao yao ya Instagram kwa maelezo yanayofanana ambapo tayari kwa Ronaldo picha hiyo imepata likes zaidi ya milioni 10 ndani ya saa moja iliyopostiwa huku post ya Messi ikiwa na likes zaidi ya milioni 8.


Watu mbalimbali wanaamini huu ni ushindi mkubwa kwa Brand ya Louis Vitton na itasaidia kuongeza mauzo ya bidhaa zao kutokana na kuwanasa Wakali hawa katika picha ya pamoja ya aso kwa uso nje ya uwanja. 
 

Post a Comment

Previous Post Next Post