UTAJIRI WA OMMY DIMPOZ TISHIO

 

MUSIC FACTS: UTAJIRI WA OMMY DIMPOZ NI TSH. 4.6 BILIONI


Ametimiza 10 ndani ya Bongofleva akiwa na albamu moja, ameshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA).


Ommy Dimpoz ambaye ni shabiki wa Simba SC na Man United alianza kuimba akiwa sekondari katika kundi lao walilolipa jina la ‘VIP’ lililoundwa na watu wanne. Bongo Music Facts inakujuza zaidi:


1. Baada ya kuimba vizuri wimbo wa Mr. Paul, Zuwena, ndipo TID akakubali kumuingiza Ommy Dimpoz ndani ya Top Band na kuungana na waimbaji wengine akiwemo Steve RnB.


Dili la kujiunga Top Band kwa mara ya kwanza alilisikia alipofika studio Sei Records ambapo Prodyuza Sendo alimwambia TID anatafuta waimbaji.


2. Wimbo anaoupenda zaidi Ommy Dimpoz kutoka kwenye albamu yake mpya, Dedication, ni ‘Moyo’, Dimpoz anaamini moyo ndio unapelekea watu kufanya mambo ambayo hata wao wenyewe hawapendi kuyafanya.


3. Msanii wa kwanza Ommy Dimpoz kutaka kumshirikisha ni AY ila hakufanikiwa, ndipo akampata Alikiba aliyesikika kwenye ngoma, Nai Nai iliyomtoa kimuziki.


Prodyuza wa ngoma hiyo, KGT ana mchango mkubwa kumshawishi Kiba ambaye ndio alikuwa ametoka kufanya kazi na R Kelly kwenye mradi wa One8 ulioachia ngoma, Hands Across The World.


4. Diamond alimshauri Ommy Dimpoz asiutoa wimbo wa Nai Nai bila kufanya video, Dimpoz hakuwa na fedha ikabidi amuombe aliyekuwa mpenzi wake kwa wakati huo, Sarah msaada ambaye alilipa gharama za video hiyo kwa Director Adam Juma.


5. Huyu ndiye msanii pekee wa Bongofleva kushinda tuzo za KTMA mara mbili mfululizo kwenye kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana, alishinda mwaka 2012 na 2013 kupitia ngoma zake, ‘Nai Nai’ na ‘Me and You’ alizoshirikiana na Alikiba na Vanessa Mdee.


6. Ommy Dimpoz alikutana na Fally Ipupa mkoani Mwanza na wakakubaliana warekodi ngoma pamoja, ila Fally alimwambia inabidi amfuate Paris, Ufaransa ambapo ndipo wimbo wao, ‘Mom Bebe’ umerekodiwa na Dimpoz hajamlipa kwa kufanya kolabo hiyo.


7. Huyu ndiye msanii pekee Bongo aliyesanishwa na wasanii wanzake katika lebo na yeye kusainisha, Ommy Dimpz alisainiwa na AY ndani ya Unity Entertainment, kisha Alikiba akamsaini RockStar Africa, naye Dimpoz akamsaini Nedy Music ndani ya Poz Kwa Poz (PKP) .


8. Show ya kwanza kubwa kufanya Ommy Dimpoz baada ya kuachia ngoma, Nai Nai, ni After School Bash iliyoandaliwa na XXL ya Clouds FM, na show yake ya kwanza Ulaya aliongozana na Alikiba.


9. Utajiri wa Ommy Dimpoz unakadiriwa kufikia Dola2 milioni (takribani Sh4.6 bilioni). Data hizi zinatoka kwake mwenyewe ambaye alitoka kimuziki mwaka 2012 na kushinda tuzo ya KTMA kama Msanii Bora Chupukizi.


10 Diamond ndiye msanii ambaye amekutana na Ommy Dimpoz kwenye ngoma nyingi zaidi bila kwa wao kushirikishana kwenye kazi zao, yaani wao hujikuta wameshirikishwa kwa pamoja na wasanii wengine.


Wamekutana kwenye ngoma kama; ‘Utamu’ ya Dully Sykes, ‘Piga Simu Remix’ ya Diva na ‘Prokoto’ ya Victoria Kimani kutokea Kenya, pia kuna ‘Leka Dutigite’ na ‘Nyumbani’ za kundi la Kigoma All Stars.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post