MAMA NA WANAE WAFARIKI WAKITOKA KWENYE MAHAFALI



Moja ya matukio yaliyojaa simanzi na huzuni ni tukio la ajali iliyoangamiza wanafamilia watatu waliokuwa wanatoka kwenye sherehe ya mahafali Kibaha mkoani Pwani.


Ajali hiyo ilitokea usiku wa Novemba 26 mwaka huu maeneo ya Kibamba jijini Dar na kubeba uhai wa mama wa familia hiyo, Immaculata Byemerwa (49) pamoja na watoto wake wawili, Jolister Byemerwa (17) aliyefanyiwa sherehe ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Gili ya Kibaha na Janeth Byemerwa (20) ambaye ni mwanafunzi aliyekuwa anasoma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.


Aliyenusurika kwenye ajali hiyo ni Albert Mrema na sasa yupo chumba cha uangalizi maalum katika Hospitali ya Mloganzila akipatiwa matibabu.


Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha ajali hiyo ya kusikitisha ni gari aina ya Prado Land Cruiser walilokuwa wanasafiria kupoteza mwelekeo kwa kuacha njia na kuangukia kwenye bonde na kusababisha janga hilo.





 

Post a Comment

Previous Post Next Post