WAFANYAKAZI WA DAVIDO WATIWA MBARONI KUFUATIA KIFO CHA MTOTO WA STAR HUYO

Kituo cha Radio cha Nigeria Info 99.3 kimeripoti kwamba Polisi wa Lagos wamewakamata Wasaidizi wa kazi za nyumbani wa Msanii Davido na wanaendelea kuwahoji kufuatia kifo cha Mtoto wa Mwimbaji huyo aitwae Ifeanyi (3) ambacho kinadaiwa kutokea kwa kuzama kwenye swimming pool.


Hata hivyo pamoja na kwamba kwenye mahojiano hayo Msemaji wa Polisi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kukataa kusema chanzo cha kifo kwa sasa, mitandao mingi ya Nigeria imeripoti kwamba amefariki baada ya kuzama kwenye bwawa hilo la kuogelea, naendelea kufuatilia zaidi ili kukuletea habari za kuaminika. 
 

Post a Comment

Previous Post Next Post