YAJUE MADHARA YA KUTOA MIMBA


 JE KUNA MADHARA YA KUTOA MIMBA⁉️


Kabla hujafiria kutoa mimba, ni muhimu kufahamu matokeo mabaya kiafya yanayoweza kujitokeza siku za mbele baada ya kufanya kitendo hichi, hasa kwenye swala zima la uzazi.


 NINI KINATOKEA BAADA YA KUTOA MIMBA?


Wanawake wengi hupata dalili hizi siku chache baada ya kutoa mimba, dalili ambazo zinaweza kuchukua mpaka siku 21 kuisha


1. ```kutokwa damu kwa week 2 mpaka 4

2.muumivu ya nyonga

3.mwili kukosa nguvu na kusinzia ovyo

4.kutapika na kizunguzungu```


MADHARA MAKUBWA YANAYOWEZA KUJITOKEZA BAADA YA KUTOA MIMBA NI PAMOJA NA:


🔆 ```majeraha kwenye mlango wa kizazi na kizazi

🔆kutokwa damu kupita kiasi mpaka kuishiwa damu

🔆mimba kushindwa kutoka yote(incomplete abortion) na hivo kuhitaji upasuaji mwingine

🔆maambukizi sugu kwenye via vya uzazi(PID)

🔆makovu kwenye tumbo la uzazi

🔆kufanyika kwa mashimo ndani ya kizazi

-mgonjwa kufariki```


MADHARA YA MUDA MREFU BAADA YA KUTOA MIMBA.


🔆 ```kujifungua mtoto kabla ya muda wake kutimia(pre-term deliveries

🔆kutoa mimba husababisha kulegea kwa mlango wa kizazi na hivo kuongeza hatari ya mimba zijazo kutoka ama kujifungua kabla ya wakati yaani chini ya week 37.

endapo mtoto atazaliwa chini ya muda wa week 37 anaweza kupata madhara ya kiafya kama matatizo ya ubongo.

🔆saratani ya matiti: Tafiti zinasema kwamba kutoa mimba kunaongeza hatari ya mwanamke kupata saratani ya matiti.

kuugua magonjwa sugu kama chlamydia na PID


🔆kupata magonjwa ya akili:

tafiti zinasema kwamba waawake wengi hupata matatizo ya akili baada ya kutoa mimba na dalili kama

kujutia kutoa mimba

sonona na msongo mkubwa wa mawazo

kupata wasiwasi kama je watashika tena ujauzito mwingine

kuona aibu na kujihisi wakosaji

kupata mawazo ya kujiua

Kama ulitoa mimba na unaanza kupata dalili hizi hapa juu, chukua hatua mapema, onana na mtaalamu wa afya ya akili kupata ushauri wa kina.````


KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO KWA SIKU ZA BAADAE BAADA YA KUTOA MIMBA.


1.Kutokana na athari ya magonjwa kama PID kwenye kizazi na mirija, inaweza kupelekea mwanamke kushindwa kushika mimba kwa siku za baadae.


2.Kwa mwanamke aliyetolewa mimba hospitali kutokana na changamoto za kiafya, hatari ya kukosa mimba kwa siku zijazo ni kubwa hasa kama mwanamke husika ana changamoto za kisukari, magonjwa ya figo, ini, moyo na mapafu na kuchanika kwa kizazi.


3.Kushindwa Kushiriki Tendo la Ndoa ipasavyo


BAADA YA KUTOA MIMBA WANAWAKE HUWEZA KUPATA CHANGAMOTO KWENYE TENDO KUTOKANA NA;


1.uke kuwa mkavu sana

2.kupungua kwa hamu ya kushiriki tendo

3.kushindwa kufika kileleni na

4.maumivu makali wakato wa tendo.


.HAYO NDO MADHARA YA KUTOA MIMBA 

GUSA HAPA KUSUBSCRIBE CHANEL YA MON JR MEDIA ILI USIPITWE 

👇👇

https://youtube.com/channel/UC7uh47xBkwNPvZKeq0YxShw

Post a Comment

Previous Post Next Post