TAARIFA KUTOKA TFF




◾Usajili wa wachezaji wa kigeni hasa kwa Klabu ambazo timu zao zinacheza mashindano ya kimataifa ulishapitishwa na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la mpira wa miguu TFF


◾Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji katika mazingira maalumu ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji hao wa kigeni ili Wawahi usajili wa shirikisho la mpira wa miguu Africa CAF


◾Wachezaji wote wa klabu hizo AZAM, SIMBA YANGA na GEITA, walishapewa leseni zao kwa ajili ya msimu wa 2022-2023 ambazo pia ndizo zimetumika kuwaombea usajili ya mashindano ya CAF 


◾Kwa mujibu wa kanuni ya 62 (1) ya ligi kuu toleo la 2022,klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12. Hivyo kutaka a kujaribu kusajili wachezaji zaidi ya idadi hiyo ni kwenda kinyume na kanuni.

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post