AMCHINJA MWENZAKO KISA SUPU



Jamal Shomari Mtepa anayekadiriwa kuwa na umri kati miaka 25 hadi 30 mkazi wa Kijiji cha Mchakama, Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi ameuwawa kwa kuchinjwa kwa kile kinachoelezwa kuwa alikunywa supu iliyokuwa imewekwa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina la Akadwii.


Inaelezwa kuwa wawili hao walikuwa marafiki na siku ya tukio hilo Oktoba 24/2022 walienda pamoja kunywa pombe na waliacha supu nyumbani ambapo Mtepa aliwahi kurudi nyumbani na kuamua kuinywa supu hiyo


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mchakama, Mohamedi Waziri Mpinga amesema marehemu Mtepa na Akadwii ni marafiki na walikuwa na tabia ya kutembeleana na muda mwingine kila mmoja alikuwa analala kwa mwenzake


“Huyu jamaa amemkata kichwa chote na kuacha sehemu kidogo ya ngozi kutenganisha kati ya kichwa na kiwiliwili”Alisema Mpinga.

Post a Comment

Previous Post Next Post