STAA WA MOVIE AJIUA KISA NI HIKI

😳😭 Vaishal Takkar(30) mwigizaji wa kike wa tamthilia za kihindi amejiua na sasa imebainika chanzo cha kujiua ni manyanyaso makali aliyokuwa akipitia toka kwa ex wake huyo ambaye licha ya kwamba baada ya kumwagana yeye alianzisha mahusiano na mdada mwingine na kumuoa lakini hakutaka Vaishal na yeye aendelee na maisha yake wala kuolewa na mwanaume mwingine  


Ex wake huyo kwa jina la Rahul licha ya kuoa akawa anataka aendelee katika mahusiano na Vaishal ambaye alikuwa hataki hivyo kuanza kumtukana kila kukicha na kuanza kumtishia kuvujisha picha zake za utupu walipokuwa pamoja kitendo ambacho kilianza kumsababishia msongo wa mawazo mrembo huyo 


Rahul pichani pia akawa anamtukana kila wakati mrembo huyo na boyfriend wake mpya aliyetaka kumuoa na kutaka kumtumia boyfriend wake mpya picha zao za utupu wakati yeye alipokuwa yupo na Vaishal. Ikapelekea mrembo huyo apatwe na msongo mkubwa wa mawazo kisha kujiua baada ya manyanyaso ya miaka 2.5 toka kwa ex wake huyo


Katika ujumbe aliouacha ambao polisi wameuoana, Vaishal amemtaja wazi ex wake huyo kuwa ndio chanzo cha yeye kukosa maisha yenye amani na kujiua kwani pia alikuwa akimnyanyasa hata kimwili, kiakili na kihisia. Pia amewasihi wazazi wake wamchukulie hatua za kisheria Rahul


Mke wa Rahul pia ametajwa kumnyanyasa mrembo huyo kwa matusi baada ya kugundua mumewe sio mwaminifu kwake bado anamtaka Vaishal ambaye hakutaka tena mahusiano nae. Kumbuka Vaishali ndie alianza mahusiano na Rahul kabla ya kuoa mdada mwingine 


Rafiki wa karibu wa Vaishal pia amekiri rafiki yake huyo alikuwa akinyanyaswa sana na ex wake hata kabla ya kuachana na alipotaka kumpa msaada Vaishal akasema atajaribu kulitatua mwenyewe. Pia amesema Vaishal alijaribu kwenda kwa mtaalamu wa saikolojia amsaidie kutokana na alichokuwa akipitia


Waigizaji wenzie akiwemo mwigizaji wa Kiume amekiri yeye pia aliwahi kuambiwa na Vaishali kuwa ex wake amekuwa sumu kwake anamnyanyasa sana na kutishia kuvujisha picha zake za utupu 


Polisi tayari wamemtia mbaroni Rahul ambaye licha ya kuoa lakini akawa bado anamuandama ex wake huyo hadi kujiua
 

Post a Comment

Previous Post Next Post