TAJIRI NAMBA 1 DUNIANI AFANIKIWA KUINUNUA TWITTER

CEO wa SpaceX na Tesla, Elon Musk Mzaliwa wa Pretoria, Afrika Kusini ambaye ni Tajiri namba moja duniani, amekamilisha ununuzi wake wa mtandao wa Twitter kwa USD Bilioni 44.


Awali Kampuni hiyo ilipinga dau lake kisha baadaye ikakubali lakini Musk akaonesha kuifuta nia yake ya kuununua mtandao huo hadi kupelekea Twitter kumpeleleka Bilionea huyo Mahakamani ili kujaribu kumlazimisha kununua Kampuni hiyo.


Elon Musk amepania kufanya mabadiliko kadhaa kwenye mtandao huo ikiwemo kulegeza masharti ya maudhui. 


Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo, Parag Agrawal na Afisa Mkuu wa Fedha Ned Segal hawako tena na kampuni hiyo na wameripotiwa kufukuzwa kazi na Musk baada tu ya kukamilisha dili hilo, Mwanzilishi mwenza wa Twitter Biz Stone amemshukuru Agrawal na Segal kwa mchango wao mkubwa katika Kampuni hiyo.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post