KICHANGA CHA MIEZI 2 AKATWA MKONO NA BABA AKE MZAZI

⚠️😳😭 Mtoto huyo wa miezi 2 amekatwa mkono baada ya kushushiwa kichapo kikali na baba yake mzazi 


Baba mtu kwa jina la Amatobi(31) alikuwa amelala ambapo mwanae huyo alianza kuangua kilio ndipo akachukua henga la plastic na kuanza kumshushia kichapo kikali mtoto huyo kwa madai alikuwa anamsumbua na kumghasi. Alimpiga hadi kumvunja mkono wa kulia. Aliposhtuka kuwa kamvunja mtoto mkono, akachukua kipange cha mti na rababendi kumfunga mfupa uliovunjika


Mama mtoto mwenye miaka 20 alikuwa ametoka kidogo ambapo aliposikia kilio kisicho cha kawaida cha mtoto wake alirudi mbio ndipo akashangaa kilichotokea kwa mshtuko. Ambapo, mume hakukawia akawafungia wote na mtoto na kuchukua simu ya mke wake ili asiweze kutoka nje Wala kuwapigia majirani kuomba msaada


Lakini, baada ya siku mbili mama mtoto alipata upenyo akachomoka ndani kwenda kuomba msaada wakaenda hospitali lakini wlikuwa washachelewa kwani mkono wa mtoto huyo wa miezi miwili ulikuw umevimba na kuharibika ilibidi mkono ukatwe kuanzia mabegani


Baba mtoto alijaribu kudhibitiwa kwa unyama huo aliofanya kwa mwanae lakini akafanikiwa kukimbia


Mke ameomba sheria ichukue mkondo wake mumewe aadhibiwe na mwanae apate haki yake kwani alichofanyiwa kisa tu kulia kama watoto wengine sio sawa


Tukio limetokea Nigeria tarehe 7 October hii, mama mtoto ametembelewa na kituo cha haki za binadamu nchini humo na waandishi wa habari wanawake, ambapo wameomba vyombo dola vimchukulie hatua mara moja mume husika huku wakisema pia mama wa mtoto kwa umri wa miaka 20 alionao ni mdogo sana kuanza kukumbana na majanga ya aina hiyo toka kwa mtu anayemuita mume 



 

Post a Comment

Previous Post Next Post