BINADAMU MCHAFU NAMBA MOJA DUNIANI AFARIKI

Z😳😭 Amou Haji(94) anayesadikika kuwa mtu mchafu zaidi duniani afariki dunia 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Irani anakotokea, Amou hajaoga kwa miaka 60 sasa na alikuwa anaamini sabuni na maji akioga vitasababisha aumwe

Chakula chake kwa kiasi kikubwa kilikuwa kichafu zikiwemo nyama zilizooza na maji alikuwa anakunywa machafu. Pia alikuwa anapenda sana kula nyama ya nungunungu(porcupine).  Alipokuwa akipewa maji safi ya kuoga na ya kunywa alikuwa hataki na kujisikia vibaya 

Alikuwa pia anapenda kuvuta sigara na kuonekana anavuta pafu za sigara zaidi ya moja kwa wakati mmoja 

Mara kadhaa alikuwa akilazimishwa na watu kuoga na kukataa, ambapo ni kama uzalendo ulimshinda miezi kadhaa iliyopita alioga na haikuchukua muda akaanza kuumwa mwishowe juzi jumapili iliyopita alifariki dunia 

Hakuwa anajulikana kuwa na familia ingawa wanakijiji walikuwa wakimuangalia

 

Post a Comment

Previous Post Next Post