MR BLUE AFUNGUKA KUWATOA KIMZIKI MASTAA HAWA WAWILI

MUSIC FACTS: Mr. Blue akili kuwatoa Alikiba na Diamond kimuziki


BAADA ya kifo cha mama yake mzazi, Mr. Blue alipanga kuachana na muziki na kwenda Uingereza kumtafuta ndugu wa baba yake wenye asili ya Sudan. Hiyo ni baada ya kushuka moyo na kukata tamaa na muziki!


Mtangazaji B Dozen alimshauri arekodi wimbo mmoja wa mwisho na ampatie, ndipo Mr. Blue akarekodi ngoma, ‘Pesa’ iliyompatia show nyingi zilizomwingiza fedha hadi kumalizia nyumba yake iliyokuwa inahitaji zaidi Sh25 milioni kukamilika. Fahamu zaidi;


1. Alianza muziki kwa kutumia jina la Dogo Lil Sameer, baadaye akaja na Lil Sameer, alipotoa wimbo wake, Blue Blue, ndipo likazaliwa jina la Mr. Blue, hiyo ni sawa na Mshikaji wake, Nyandu Tozzy ambaye alianza muziki na jina la Dogo Hamidu.


2. Ngoma ya Mr. Blue, ‘Baki na Mimi’ ameiandika kwa ajili ya mke wake, Waheeda ambaye kwa mara ya kwanza walikutana club ya Bilcanas, Dar es Salaam, na tayari wana watoto watatu.


3. Abby Skills ndiye aligundua kipaji cha Mr. Blue kisha akamkutanisha na Dully Sykes ambaye ndiye alimpeleka studio kwa DJ G Lover (Guru) na kuanza kurekodi hadi akatoka kimuziki.


4. Wimbo wa Mr. Blue, Mapozi aliupewa na Abby Skills na ulirekodiwa, G Records, na wimbo wa Abby Skills, ‘Mimi Na Wewe’ aliupewa na Mr. Blue. Ni kama walifanya mabadilishano ya ngoma.


5. Mr. Blue ndiye aligundua kupaji cha Young Dee, naye akampeleka kwa Dully Sykes ambaye alimpa jina hilo (Young Dee) kisha kumpeleka studio kwa Lamah, Fishcrab ndipo akatoka kimuziki.


6. Hadi sasa Mr. Blue hajawahi kushinda tuzo Bongo, zile za Tanzania Music Awards (TMA), hiyo ni sawa na wakali wengine kama TID, Dully Sykes na Juma Nature. Usishange maana Snop Dogg na ukali wake hajawahi kushinda tuzo ya Grammy licha ya kutajwa kuwania mara 17.


7. Mr. Blue anapenda sana kuzikiliza muziki wa Rege na ndio chanzo cha kuanza kutumia ‘sauti ya kukwaruza’ kwenye muziki wake na hilo alishauriwa na Nyandu Tozzy.


8. Baada ya kifo cha Prodyuza Roy mwaka 2008 ndipo Mr. Blue alianza kuacha kuimba na kujikita kwenye Rap, anaamini Roy waliyefanya kazi pamoja G Records ndiye alikuwa anampatia vizuri pindi anapoimba.


9. Mr. Blue aliletewa Alikiba na Abby Skills na kuulizwa kuhusu uwezo wake, Blue alijibu ana uwezo mzuri kimuziki ndipo wakarekodi pamoja wimbo, Maria ambao ulimtoa Alikiba kimuziki.


Baadaye tena Blue akaletewa Diamond Platnumz na Papa Misifa na kumuuliza kama anaweza kumtoa, Blue akajibu Diamond ana uwezo mzuri na anamfahamu toka muda, ndipo Diamond akatolewa. Na Alikiba na Diamond wote wamewahi kushirikiana na Mr. Blue kwenye nyimbo zaidi ya mbili.


10. Fedha ya kwanza nyingi Mr. Blue kulipwa kwenye muziki ni Sh1500,000 katika show aliyofanya Mwanza ambapo aliambatana na Joti na Mpoki, ni kipindi Wachekesaji hao bado hawajawa maarufu chini ya kundi la Orijino Comedy.
 

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post