UJUMBE WA MAMA SALMA KIKWETE KWA MUMEWE ALIYETIMIZA MIAKA 72

Wasichana walimbabaikia Kikwete - Mama Salma


Ikiwa leo Rais mstaafu Dkt.Kikwete anatimiza miaka 72, Mama Salma amegusia kuhusu safari yao ya mahusiano na ndoa ambapo akihojiwa na Clouds Media Group amesema hakuwa akifahamiana na Kikwete kabla na kwa mara ya kwanza walikutana kwenye mkutano wa kuhamasisha siasa uliofanyika chuoni kwao


“Mimi nilikuwa naimba kwenye kwaya , yeye amekuja kuhamasisha vijana masuala ya siasa kwahiyo nilitimiza jukumu langu la kuimba na yeye akaweka siasa zake jukwaani shughuli ikaisha" amesema na kuongeza


“Basi walivyoondoka na kamati yake ya siasa na sie tukaendelea na shughuli zetu, tuliporudi bwenini mazungumzo ya wasichana wote yalikuwa ni kumhusu yeye na muonekano wake akisifiwa kuwa mzuri(mtanashati) hata hivyo Mungu humpa amtakaye baada ya muda tukaoana, “ amesema Salma Kikwete alipokuwa akihojiwa na Clouds Media Group
 

Post a Comment

Previous Post Next Post