WASANII WA KIKE WA BONGO WANAFEKI MAISHA, HALI ZAO NI NGUMU HADI HURUMA;NICOLE


 

WASANII WA KIKE WA BONGO WANAFEKI MAISHA, HALI ZAO NI NGUMU HADI HURUMA;NICOLE 

Mlimbwende mwenye shepu la Batamzinga bongo, Nicole Joyce Berry, maarufu kama Nicole amewahi kusema wasanii wengi wa kike wa Tanzania wana hali ngumu za kutisha majumbani mwao, tofauti na wanavyojinadi Instagram na Facebook kuwa wana maisha mazuri, wana magari, wanalipa kodi bei ghali kitu ambacho ni uongo wana followers wengi lakini wanalia njaa ukikutana nao lazima wakuombe pesa za bia na mafuta ya gari.

Nicole ambaye licha ya kumiliki Saloon kubwa Mbezi beach lakini analima na sasa amejikita kwenye uigizaji ambapo anaonekana kwenye tamthiria ya Huba.

Nimeyakumbuka maneno ya Nicole baada ya kuona Aggy wa Uchebe alivyojinadi leo Wasafi kuwa anatumia pesa zaidi ya milioni sita kwa siku mbili, mimi naona kuna muda hawa kinadada wapuuzwe hata wanyimwe interview, maana hakuna la maana wanaloliongea zaidi ya kupotosha jamii hasa watoto ambao nao watatamani kuingia kwenye sanaa wakizani kuna maisha mazuri alafu wakutane na vitu tofauti.

Post a Comment

Previous Post Next Post