RAFIKI WA ANJERA ATOA MADAI MAZITO KUHUSU ANJERA


 😳 Rafiki wa Anjella atoa madai mazito kuhusu Anjella


Akihojiwa na Maximum TV, Aunt Lulu amemkaanga Anjela na kufichua maovu yote ya mwanadada huyo anayetajwa kuwa na hali ngumu na tatanishi kwa sasa.


Aunt Lulu amesema aliamua kumsaidia Anjela baada ya kuona anahangaika huku na kule kupata sehemu ya kuishi kutokana na kukosa kodi na pesa ya kula, akaamua kuchukua jukumu la kumsaidia kwa kila kitu kuanzia mavazi hadi chakula lakini malipo yake anajuta kumsaidia.


"Nilimkuta yupo kwenye hali mbaya sana na Menejimenti yake walikuwa hawamjali hata kujua yuko wapi, Anjela ni msiri sana, nilimkuta ana ujauzito wa miezi mitano ambao alikuwa anataka kuutoa maana alisema Harmonize akingundua atavunja makataba, nilimshauri asitoe lakini hakunisikiliza akatoa".


"Hadi sasa mimi na yeye tumekosana kabisa baada ya kuniambia mimi ndiyo nilivujisha voice zake kwa Mange Kimambi wakati tulivujisha wote ingawa mimi ndo Mange alikuwa ananitumia pesa, kitendo cha yeye kusema nimesambaza voice zake kimenikosesha madiri mengi watu wamenichukia sana, kwanza Anjela ni mbaya sana ana dharau sana"; ameongea Aunt Lulu.


Ameongeza kwa kusema Anjela anatumia mguu wake kama siraha ya kuonekana mwema, lakini Anjela bangi amevuta na ni tapeli wa kutupwa amedhurumu watu wengi sana wakiwemo madansa wake, yani kwa jeuli aliyonayo hawezi kupata msada kamwe duniani labda msada wake aungoje kwa Mungu



Post a Comment

Previous Post Next Post