HARMONIZE BAADA YA BURNA BOY NAFUATA MIMI

Harmonize; ni msanii mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye anazidi kutilia mkazo kuwa kwa sasa msanii wa Nigeria, Burna Boy ndiye msanii mkubwa duniani.


Harmonize anasema kuwa, wapambanaji pekee ndiyo wanaweza kumuelewa huku akijitaja kuwa yeye ndiye anayefuata baada ya Burna Boy.


Harmoniez anasema kuwa, kwa sasa Burna Boy ndiye msanii mkubwa huku akitaja baadhi ya matukio aliyojifunza kutoka kwa staa huyo kipindi akiwa Lagos, Nigeria.


Konde Boy anasema kuwa, hakuwahi kumsikia Burna Boy akimzungumzia mtu ambaye hayupo kwa wakati huo na hakuwahi kumsikia akijisifia juu ya mafanikio yake na tuzo alizonazo.


Pia Harmonize anasema kuwa, hawezi kuficha kusema ukweli kwamba kwa sasa Burna Boy ndiye msanii namba moja.


Anasisitiza kuwa, kila mtu anaweza kutaja jina la staa anaeona yeye ndiye namba moja, lakini watu wasisahau kuwa yeye ndiye anayefuata baada ya Burna boy

 

Post a Comment

Previous Post Next Post